KONGAMANO LA
KIMATAIFA LA KISWAHILI
"Ustawi wa Kiswahili Duniani: Tulikotoka, Tulipo na Tuendako"
TAREHE 7-10 NOVEMBA, 2024 | HAVANA, CUBA
Kuhusu Kongamano
Kongamano la Kimataifa la Kiswahili ni tukio lenye hadhi ya kidunia, linaloletwa kwetu kwa hisani ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Cuba na Wadau wa Kiswahili Duniani kwa lengo la kukuza, kuenzi na kueneza lugha ya Kiswahili.
Karibu sana! ukutane na wataalamu, wakereketwa, na wadau wa Kiswahili toka sehemu mbalimbali Duniani. Utafurahi kutangamana nao na kuwa sehemu ya familia kubwa ya wasemaji wa Kiswahili. Jitayarishe kwa siku nne za mijadala, mafunzo na shughuli za Utamaduni na Utalii. Usikose fursa hii adimu, Jisajili sasa!
Wapi?
Havana, Cuba
Lini?
Alhamisi hadi Jumapili
Novemba 7-10, 2024
Watashiriki
Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Mhe. Dkt. Damas Daniel Ndumbaro
Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo (WUSM)
Mhe. Humphrey H. Polepole
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Havana, Cuba
Ratiba ya Kongamano
UFUNGUZI WA KONGAMANO
KUWASILI KWA WASHIRIKI & BURUDANI
Burudani itatolewa na Janeth Band - Son de Primera
MGENI RASMI KUWASILI
Programu itahusisha uimbaji wa nyimbo za Taifa kwa Taifa la Kuba na Tanzania
UTAMBULISHO
Utambulisho utafuatiwa na burudani ya Ushairi kutoka kwa Abdurahman Famau kutoka Tanzania
SALAMU ZA KITAIFA NA HOTUBA YA MGENI RASMI
Salamau za Rais wa Kuba, zitatolewa na Waziri wa Elimu ya juu wa Kuba
Hotuba ya Mgeni Rasmi Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, itatolewa na Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo.
UZINDUZI WA KAMUSI
Kamusi ya lugha ya Kihispaniola na Kiswahili itazinduliwa, kisha kufuatiwa Burudani kutoka kwa Siti and the Band
CHAMCHA & MAPUMZIKO
Kisha viongozi kuelekea katika Bustani ya African Heros kwa ajili ya uzinduzi wa sanamu la Nyerere
UWASILISHAJI WA MAKALA
Uwasilishaji wa makala kuendelea ukumbini
UWASILISHAJI MAKALA NA USIKU WA MSWAHILI
CHAI & KUJISAJILI
Washiriki wote watahusika
UWASILISHAJI MAKALA NA MIJADALA
Wawasilishaji waliopangwa wataongoza programu
CHAMCHA NA MAPUMZIKO
Watu wote
UWASILISHAJI WA MAKALA NA MIJADALA
Muendelezo wa uwasilishaji makala
SALAMU ZA BUNGE
Kutoka kwa Mhe. Husna Sekiboko (Mb) Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na Elimu
HAFLA YA UFUNGAJI
Mgeni Rasmi ataongoza
MAANDALIZI YA USIKU WA MSWAHILI
Washiriki kupewa muda wa kujiandaa kwa ajili ya programu ya usiku wa Mswahili
KUWASILI KATIKA UKUMBI WA GRAN MUTHU HABANA
Washiriki kuanza kuwasili katika ukumbi wa Gran Muthu Habana tayari kwa kuanza programu ya usiku wa Mswahili
HAFLA YA USIKU WA MSWAHILI
Programu ya Usiku wa Mswahili kutekelezwa kwa kadri ya ratiba yake itakavyoongoza
UFUNGAJI KONGAMANO NA USIKU WA MSWAHILI
Washiriki kuwasili katika ukumbi wa Gran Muthu Habana
Washiriki wote wa kongamano
MGENI RASMI KUWASILI
Mgeni rasmi Mhe. Riziki Pembe(Mb) kuwasili kisha kupata burudani kutoka kwa Siti & The Band
NENO LA UKARIBISHO
Kutoka kwa Bw. Gerson Msigwa, Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo
ONESHO LA MAVAZI YA KHANGA SEHEMU YA I
Kisha kufuatiwa na burudani kutoka kwa Abdurahman Famau (Mshairi)
ONESHO LA KHANGA SEHEMU YA II
Kisha kufuatiwa na hotubu ya Mgeni rasmi Mhe. Riziki Pembe(Mb) Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto pamoja na burudani kutoka kwa Siti & The Band
ONESHO LA MAVAZI SEHEMU YA III: KANZU, KOFIA, UBEBAJI BAKORA
Kisha kufuatiwa na neno la shukrani kutoka kwa Bi. Fatma Hamad Rajab
BURUDANI YA MUZIKI NA KUFUNGA
Kupata burudani ya muziki kutoka kwa Siti & The Band, Chakula na Kufunga.
Eneo la Kongamano
Picha mbalimbali kuonesha mandhari ya jiji la Havana mahali ambapo kutafanyika Kongamano la Kimataifa la Kiswahili.
Havana, Cuba
Havana ndio mji mkuu na mkubwa zaidi wa Cuba. Ni moyo wa Mkoa wa La Habana, Havana ni bandari kuu ya nchi na kituo cha biashara. Ni jiji lenye watu wengi zaidi, kwa eneo ndio mji mkubwa kuliko yote, na wapili kwa ukubwa katika ukanda wa Karibiani. Idadi ya watu katika Jiji la Havana inakadiriwa kufikia ni 2,163,824, na ukubwa wa eneo lake ni 728.26 kmsq.
Clínica Central Cira García
Calle 20 NO. 4101 esq. a Av. 41 Miramar, La Habana, Cuba
Hospital Hermanos Ameijeiras
Calle, # 701 San Lazaro, La Habana 10400, Cuba
International Center for Neurological Restoration (CIREN)
Calle 216 esq. 13 Reparto Playa, Siboney, La Habana, Cuba
Hoteli
Baadhi ya Hoteli zinazopatikana katika jiji la Havana
Habari Picha
Bofya kwenye picha ili kuangalia kwa ukubwa picha za Kongamano
Wahisani
Kongamano la Kimataifa la Kiswahili ni tukio lenye hadhi ya kidunia, linaloletwa kwetu kwa hisani ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Cuba na Wadau wa Kiswahili Dunianit
TAARIFA ZA SAFARI
Wadau wote wa kiswahili ambao wamekamilisha taratibu za safari kuelekea Kuba kuhudhuria kongamano hili jijini Havana, kamati inawaalika kuandikisha taarifa zenu za safari kupitia fomu iliyopo hapa chini.
KONGAMANO LA KIMATAIFA LA KISWAHILI JIJINI HAVANA, NCHINI CUBA
7-10 /NOVEMBA, 2024
- Usijaze fomu hii zaidi ya mara moja.
- Taarifa zako zitatumika kwa ajili ya kuratibu ushiriki wa Kongamano la Kimataifa la Kiswahili jijini Havana, nchini Cuba.
Mawasiliano
Waweza kutoa maoni yako au kuwasiliana nasi kupitia:-
Anuani
Kongamano la Kimataifa la Kiswahili 2024
Miramar-Playa, Havana, Cuba
Tupigie Simu
+53 7204 1075-77 (Cuba)
+255 755-458854 (Tanzania)
Tuma Baruapepe
havana@nje.go.tz(Cuba)
km@bakita.go.tz(Tanzania)
Machapisho
Machapisho mbalimbali kuhusu Kongamano





